Siku za hivi karibuni maelfu ya watu walishuhudia ndoa ya Mwalimu Peter Edson wa kwaya ya Hekima ambaye alimuoa Mwimbaji na solo wa miaka mingi wa kwaya hiyo Jackline Nnosye Kasisika.
Hakika siku hiyo ilikuwa ni ya baraka na shangwe tele.Hekima kwaya na wadogo zetu wa New Hope tuliambatana naye hadi ukumbi wa Istana mara baada ya ndoa yake kufungwa katika kanisa la Moravian Ushirika wa Kinondoni.
Kwa pamoja tunakutakia amani ya kimungu mwalimu Peter uishi kwa amani, ndoa yako iwe chanzo cha mafanikio na kumjua Mungu zaidi na zaidi.ubarikiwe sana