Siku za hivi karibuni Mtumishi wa Mungu Agatha Mwangaba alifunga pingu za maisha na ndugu Hebron Makalula, ndoa yake ilifungwa na baba askofu Cheyo pale kanisa la Moravian Ushirika wa Mabibo.hakika tulishuhudia wema wa Mungu ukituzunguka.
Mara baada ya harusi hiyo katika ukurasa wake wa Uso Kitabu(Facebook) mtumishi huyu aliandika jambo jema ambalo kama vijana wengine wanotarajia kufunga ndoa siku za usoni wakilizingatia wanaweza kunufaika nalo, alisema kuwa kuna maisha baada ya ndoa, akimaanisha kuwa watu wengi wamekuwa wakitumia fedha nyingi kuandaa harusi bila kujua kuwa wanapomaliza harusi yapo maisha mengine.huu ni wito wake tu mtumishi wa Mungu kwetu.ubarikiwe Mwinji
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment