Kuna mlima mrefu sana tupokuupanda, Mungu ameendelea kutufundisha kila inapoitwa leo tunamshukuru Mungu kwa kazi tunayoendelea kuifanya studio kwa ajili ya kutengeneza albamu yetu ya tatu ya Hekima kwaya, kwa kweli tumemuona Mungu akifanya nasi, kwa wanaojua habari za studio wanaelewa, labda kama lengo lenu si kuwafikia watu wengi ili wakutane na injili ya Mungu, lakini kama lengo ni kuwafikia watu wengi iwezekanavyo yahitaji kujitoa sana katika kazi hii, tunazidi kuwaomba maombi yenu.mbarikiwe.matukio katika picha yalikuwa hivi
|
Waimbaji sehemu ya waimbaji wa Hekima Kwaya wakiwa studio hivi karibuni, hapa Catherine anamshauri kitu Mwalimu Peter. inapofika sehemu lazima kuwasikiliza waimbaji huo ndiyo ualimu mwema, hapa nadhani mbinu binafsi ilihitajika. |
|
Mwalimu Peter Hapa anatoa maelekezo, namna waimbaji wanavyopaswa kufanya, tunamshukuru Mungu kwa ajili ya Mwalimu huyo anayejitoa kufanya kazi ya Mungu |
|
Baadaye Vocal ikaanza chezea studio hapa Mwalimu akijaribu kusisitiza jambo zaidi |
|
Sauti ya Kwanza wakiwajibika vilivyo, ni sehemu tu ila tunamshukuru Mungu kazi nzuri ilifanyika |
No comments:
Post a Comment