AD (728x90)

  • 2793 Pine St

    2793 Pine St

    Nulla facilisi. Cras blandit elit sit amet eros sodales, non accumsan neque mollis. Nullam tempor sapien tellus, sit amet posuere ante porta quis. Nunc semper leo diam, vitae imperdiet mauris suscipit et. Maecenas ut neque lectus. Duis et ipsum nec felis elementum pulvi...

  • 1100 Broderick St

    1100 Broderick St

    Nulla facilisi. Phasellus ac enim elit. Cras at lobortis dui. Nunc consequat erat lacus, a volutpat nisi sodales vitae. Phasellus pharetra at nulla in egestas. Vestibulum sit amet tortor sit amet diam placerat tincidunt sit amet eget lorem. Phasellus ...

  • 868 Turk St

    868 Turk St

    Nulla facilisi. Phasellus ac enim elit. Cras at lobortis dui. Nunc consequat erat lacus, a volutpat nisi sodales vitae. Phasellus pharetra at nulla in egestas. Vestibulum sit amet tortor sit amet diam placerat tincidunt sit amet eget lorem. Phasellus posuere posuere fel...

  • 420 Fell St

    420 Fell St

    Sed at vehicula magna, sed vulputate ipsum. Maecenas fringilla, leo et auctor consequat, lacus nulla iaculis eros, at ultrices erat libero quis ante. Praesent in neque est. Cras quis ultricies nisi, vitae laoreet nisi. Nunc a orci at velit sodales mollis ac ac ipsum. Na...

Feature Top (Full Width)

Latest Updates

Monday, May 13, 2013

Hata hapa tulipofika ni kwa neema yako bwana Yesu

Kuna mlima mrefu sana tupokuupanda, Mungu ameendelea kutufundisha kila inapoitwa leo tunamshukuru Mungu kwa kazi tunayoendelea kuifanya studio kwa ajili ya kutengeneza albamu yetu ya tatu ya Hekima kwaya, kwa kweli tumemuona Mungu akifanya nasi, kwa wanaojua habari za studio wanaelewa, labda kama lengo lenu si kuwafikia watu wengi ili wakutane na injili ya Mungu, lakini kama lengo ni kuwafikia watu wengi iwezekanavyo yahitaji kujitoa sana katika kazi hii, tunazidi kuwaomba maombi yenu.mbarikiwe.matukio katika picha yalikuwa hivi
Waimbaji sehemu ya waimbaji wa Hekima Kwaya wakiwa studio hivi karibuni, hapa Catherine anamshauri kitu Mwalimu Peter. inapofika sehemu lazima kuwasikiliza waimbaji huo ndiyo ualimu mwema, hapa nadhani mbinu binafsi ilihitajika.

Mwalimu  Peter Hapa anatoa maelekezo, namna waimbaji wanavyopaswa kufanya, tunamshukuru Mungu kwa ajili ya Mwalimu huyo anayejitoa kufanya kazi ya Mungu

Baadaye Vocal ikaanza chezea studio hapa Mwalimu akijaribu kusisitiza jambo zaidi

Sauti ya Kwanza wakiwajibika vilivyo, ni sehemu tu ila tunamshukuru Mungu kazi nzuri ilifanyika

Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu

Tunakila sababu za kumshukuru Mungu wetu aliye hai kwa sababu siku zote ameendelea kuwa upande wetu, si kwamba sisi ni wakamilifu sana la hasha bali ni kwa neema yake tu tumeendelea kuuona mkono wake ukifanya kazi pamoja nasi.tuzazidi kuwashukuru ndugu zetu wote kwa ushirikiano wenu wa hali na mali wa kuifanya Hekima kwaya iendelee kumtumikia Mungu wetu aliye hai.
Sehemu ya vijana wa hekima kwaya wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza ibada ushirikani Kinondoni

Wadada wa Hekima wakiwa katika picha ya pamoja, hakika tunabarikiwa sana na wadada hawa

Haya sasa Joseph Luliko Lwakeghe Minga, Meniford pamoja na Chris wakiwa katika picha ya pamoja walipomaliza Ibada

Hapa ni dada zetu Bumi Malema na Sekela Mwaipopo, kwa kweli tunamshukuru Mungu sana kwa ajili yao wamekuwa sehemu ya mafanikio katika kundi letu.

Thursday, April 4, 2013

Kumtumikia Mungu inalipa, Dodoma town Choir

Mungu awabariki watumishi wa Mungu, hakika kazi yenu si bure, iweni hodari katika kutenda mambo mema zaidi na zaidi.Ashukuriwe Mungu awapaye kibali cha kumtumikia

Tuesday, April 2, 2013

Agatha Mwangaba: Kuna maisha baada ya ndoa

Siku za hivi karibuni Mtumishi wa Mungu Agatha Mwangaba alifunga pingu za maisha na ndugu Hebron Makalula, ndoa yake ilifungwa na baba askofu Cheyo pale kanisa la Moravian Ushirika wa Mabibo.hakika tulishuhudia wema wa Mungu ukituzunguka.

Mara baada ya harusi hiyo katika ukurasa wake wa Uso Kitabu(Facebook) mtumishi huyu aliandika jambo jema ambalo kama vijana wengine wanotarajia kufunga ndoa siku za usoni wakilizingatia wanaweza kunufaika nalo, alisema kuwa kuna maisha baada ya ndoa, akimaanisha kuwa watu wengi wamekuwa wakitumia fedha nyingi kuandaa harusi bila kujua kuwa wanapomaliza harusi yapo maisha mengine.huu ni  wito wake tu mtumishi wa Mungu kwetu.ubarikiwe Mwinji

Peter&Jackline: Ilikuwa ngumu sana kuandaa Mungu amefanya mwenyewe

Siku za hivi karibuni maelfu ya watu walishuhudia ndoa ya Mwalimu Peter Edson wa kwaya ya Hekima ambaye alimuoa Mwimbaji na solo wa miaka mingi wa kwaya hiyo Jackline Nnosye Kasisika.

Hakika siku hiyo ilikuwa ni ya baraka na shangwe tele.Hekima kwaya na wadogo zetu wa New Hope tuliambatana naye hadi ukumbi wa Istana mara baada ya ndoa yake kufungwa katika kanisa la Moravian Ushirika wa Kinondoni.

Kwa pamoja tunakutakia amani ya kimungu mwalimu Peter uishi kwa amani, ndoa yako iwe chanzo cha mafanikio na kumjua Mungu zaidi na zaidi.ubarikiwe sana

Makamu Mwenyekiti wa Hekima Kwaya, Mungu hajatuacha

Makamu mwenyekiti wa kwaya ya Hekima Mrs Sara Minga Makalla akiwa katika uimbaji siku za hivi karibuni, tumeshuhudia baraka kutoka katika kinywa cha dada huyu.Mungu aendelee kukupa hekima zaidi na zaidi, pia akubariki wewe na familia yako, elewa kuwa kazi unayoifanya si bure inalipa

Nsaji:Tukijipanga sawasawa Mungu hawezi kutuacha

Mwenyekiti wa Kwaya ya Efatha Nsaji, Akimwabudu Mungu wake aliye hai, Kwa kweli Mungu anamtumia sana huyu jamaa, Hekima kwaya tunadiliki kutamka neno la baraka kwa ajli yake, wengi wamebarikiwa na kumrudia Mungu na  pia wengine kutamani kuishi maisha ya huyu jamaa.Hii ni sifa njema na iliyotukuka.Mungu akubariki sana ndugu yetu Nsaji elewa kuwa umebeba watu wengi nyuma yako kaza mwendo bado kuna tumaini.

Tuesday, August 28, 2012

Majembe Kinondoni Moravian wakiwa katika pozi

Waimbaji wa kwaya kuu Kanisa la Moravian Ushirika wa Kinondoni wakiwa katika picha ya pamoja, Jumapili ijayo kwaya hiyo itakuwa na sikukuu yake ya uimbaji kijimbo, kwa pamoja hekima kwaya na wadau wote tunawatakia maandalizi mema

Monday, July 16, 2012

Mwimbaji wa Hekima amvalisha pete ya uchumba mwimbaji mwenzake siku ya kutoa Mahari

Kupeana bila uchoyo ndiyo wajibu, Martha na Joseph wakila keki kwa staili yake huko mbozi ambapo Joseph alijitosa mwanawane kupeleka mahari, Mugnu awabariki sana
Joseph Samson akimvika pete ya uchumbaji mwimbaji solo wa Hekima Martha Msyani baada ya kutolewa mahari, ilikuwa njema sana, tunamshukuru Mungu kwa uaminifu wake

Muimbaji wa kwaya ya Hekima Joseph Samson akipata kipande cha Keki mara baada ya kumaliza shughuli ya kutoa mahari kwa binti Martha Msyani, hekima kwaya tunawapongeza kwa hatua hiyo

Pozi hili waimbaji wa Hekima kwaya martha na Joseph wakiwa katika pozi la pamoja kwenye sherehe ya kutoa mahari, mchakato wa ndoa yao utaanza siku za karibuni, hekima kwaya tunawapongeza kwa hatua waliyofikia Mungu awabariki



Matukio zaidi ya picha Ushirika wa Sayuni Moravian

Waimbaji wa kwaya kuu ya Jimbo wakijiandaa kwa ajili ya maandamano ya kuzindu ushirika mpya wa Sayuni Mohravian, uliopo maeneo ya Boko

Mwenyekiti wa Kanisa la Moravian Jimbo la Mashariki Mchungaji Fumbo akiwaongoza maelfu ya watu waliohudhuria kuanzishwa kwa ushirika mpya wa Sayuni eneo la Boko Jijini Dar es Salaam

Makamu Mwenyekiti wa Jimbo  baba Mchungaji Saul Kajura akiinamisha Chini waka ti wa maombi yaliyofanywa na Mke wake

Mwenyekiti wa Jimbo Mch Fumbo akizindua nyumba ya Mchungaji iliyokamilika kwa sehemu  ushirikani hapo

Matukio ya picha uzinduzi wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Sayuni

Joseph Samson na Jackline Kasisika wakiwaongoza wana Hekima kwenye maandamano kabla ya kuzindua Ushirika Mpya wa Sayuni

Huyu ni mama Mwaipasi hakika tunabarikiwa naye sana kwa kazi yake nzuri, katika uzinduzi huo wakinamama wa Moravian Kinondoni hawakuwa nyuma, mbarikiwe sana wakinamama

Hekima kwaya wakifanya vitu vyao

Mchungaji Saul Kajura akimbariki mtumishi wa Mungu Mwnjilisti Ndefula la mkewe kuwa wainjilisti rasmi wa Ushirika huo

Wednesday, June 27, 2012

Mungu akiwa upande wetu, watoto wetu watapona

Baba yetu wa Kiroho Mch. Israel Kabuka akifuatilia kwa umakini mkubwa ibada hiyo, pembeni ni muhubiri wa siku hiyo ambaye alitoa wito kwa wakristo kuwa na roho ya huruma katika jamii lakini pia kuwaombea sana watoto

Mahubiri yakiendelea, tulibarikiwa sana na mama huyu

Kwaya kuu nao walikuwepo, wakifanya kazi kama kawaida, wiki ijayo wanatarajia kuanza kufanya rekodi ya video

Wakina mama waombolezaji wanalibeba kanisa kimaombi

Utulivu mahakamani, aaaaaa nononono utulivu ibadani, umeonaeeeeeeeee

Wapi mama mwaipaja Soloo, ulitokaje aiseee wewe ni mkaliii bana, tulibarikiwa sana na wewe siku ya sherehe ya umoja wa kinamama

Haya sasa oooh uzeee Mwesho Ant Tona, wapi mama Mwaipasi, utawataka mwenyewe, tunabarikiwa sana na mama zetu hawa Mungu awabariki na aendelee kuwalinda daima

Wakina mama Moravian Kinondoni waaswa kusaidia yatima na wajane

Katika siku za hivi karibuni kanisa la Moravia liliazimisha sikukuu ya Wakinamama, Kanisa la Moravian Kinondoni pia walikuwepo katika kuhakikisha kuwa wanatekeleza sera na kanuni za kanisa.Sherehe zilianza mapema asubuhi jumapili iliyopita huku wakinamama wakiwa wamevalia sare zao nyeupe, hakika tuliuona utukufu wa Mungu

Monday, May 28, 2012

Mchungaji Kabuka akasema Kijana ni lazima aufurahie ujana wake

Mch.Conjester Mpanda akiwajibika vilivyo katika moja ya nyimbo kwenye sikukuu hiyo, aisee huyu dada Mungu anamtumia vilivyo.

Hawa ndiyo Magwiji wa uimbaji Kinondoni KWAYA KUU ambao hadi leo wanaendelea kutunza mila ya kimoravian yaani kupiga mapigo na ile Fimbo wenyewe hupenda kuiita "Baton"

Aiseee tunabarikiwa sana na Harvest Kwaya ni kwaya ambayo imeanzishwa hivi karibuni katika kanisa letu lakini tunashuhudia kuwaona Mungu akifanya kazi pamoja nao, Mungu ambariki sana muanzilishi wa maono haya baba yetu Mwasikili aka wa Mujini

Hapa ni baba wetu wa kiroho Mchungaji  Israel Kabuka aktoa baraka katika ibada ya kwanza.Hakika tunabarikiwa sana baba yetu huyu wa kiroho kinondoni tunapenda kumuita Mutu ya watu.babaaaaaaaaaa amani kwako

Matukio zaidi katika picha kwenye sherehe ya vijana Moraviank

Kutoka kulia ni Mtunza hazina wa Vijana Moravian Mrs Rehema Eginga, Mwenyekiti wa Vijana Dk Fredrick Mwakibinga na mama Mlezi wa vijana MAMA Kapalala

Waaumini wakifuatilia kwa makini Sherehe hizo jijini dar es salaam

Makamu Mwenyekiti wa Vijana Ayub Mbalazi akisoma Risala kwa Mchungaji iliyoelezea mambo yaliyofanywa na yatarajiwayo kufanywa, nyuma ni mchungaji Kabuka akiandika yanayojiri ndani ya hotuba

Mchungaji wa kanisa la Moravian Ushirika wa Kinondoni Kushoto Pastor Kabuka, akiwa na Mgeni wake kutoka katika kanisa la Anglikan ambaye pia ni mkufunzi wa chuo cha St Max  cha jijini Dar es salaam

Eeee Mungu tunakushukuru kwa kufanikisha sikukuu ya Vijana

Si kwamba  hapa wanamuomba kitu mto noo ni stepu jamani

kaeni tayari okey Goooooooooo

Kazi ikiendelea kanisana

Kutoka kushoto ni Martha Msyani, Adelina Mtafya, Bumi Peter, Mch.Conjester Mpanda na Nnosye Kasisika wakiwajibika vilivyo jukwaani, aiseee tulimuona Mungu akifanya kazi pamoja na sisi

ITEM LIST

  • BIBLE

ITEM LIST

  • BIBLE

Feature (Side)

© 2013 HEKIMA KWAYA MORAVIAN-KINONDONI . All rights resevered. Designed by Templateism