AD (728x90)

Tuesday, July 12, 2011

Rasilimali watu katika ustawi wa kanisa la Moravian

Hakika ndugu zangu ibada ya jumapili iliyopita tuliushuhudia upako wa Mungu ukisema nasi katika masuala ya uwakili mwema.Wapo baadhi ya watu wanazani kuwa uwakili upo katika kutoa fedha tu, lakini jumapili hii iliyopita, mtumishi wa bwana Mr Mwakibinga ambaye ni afisa miradi na  maendeleo wa jimbo la misheni mashari na zanzibar aliweza kufafanua jambo hili kwa umakini wa hali ya juu.


katika mahubiri yake alisema wakili mwema ni yule mtu anayeweza kupangilia mambo yake yakawa yanafanyika kwa utaratibu lengo likiwa ni kukuza uelewa chumi uaminifu katika maisha yake ya kila siku.Mr Mwakibinga ambaye ni mkristo mshiriki wa kanisa la Moravian ushirika wa Tabana anaeleza kuwa wapo baadhi ya wakristo ambao wamemtumikia Mungu kwa uwakili mwema hivi sasa wanapeta kimaisha.

Alisema kwa kuwa wameitambua mbinu hiyo ya ibilisi ya kuwasahaulisha waumini kwa kutojua wajibu wao katika kanisa, Mwakibinga alisema kuwa hivi sasa wanakusudia kupitisha orodha ya wakristo wote katika jimbo na kutambua shughuli wanazozifanya ili taaluma zao ziweze kulisaidia kanisa.

"Ndugu zangu leo hii tukipitisha karatasi na kutaka kujua watu wanataaluma gani katika kanisa utashangaa sana, utakuta madaktari, wahandisi, wachoraramani, waandishi wa habari, wafanyabiashara wakubwa na mambo mengi, lakini rasilimali watu hii kanisa limekuwa haliitumii ipasavyo ili kustawisha kanisa" alisema Mr Mwakibinga.

alisema wakati umefika kwa makanisa kuachana na dhana ya kutegemea ufadhili kutoka nje yan nchio badala yake wakristo wajibidishe katika kuhakikisha kuwa wanajitoa kwa kila hali katika kazi za kanisa ili kuleta heshima ya kristo ndani na nje ya kanisa.

No comments:

© 2013 HEKIMA KWAYA MORAVIAN-KINONDONI . All rights resevered. Designed by Templateism