AD (728x90)

Tuesday, June 7, 2011

Tujadili huduma ya Uimbaji wa nyimbo za Injili

Kuna mada inayoelezea kuwa Uimbaji wa mtu binafsi (Single Artist) pamoja na ule wa kutumia Play Back katika kwaya zetu ni dhana iliyoandaliwa na Mwovu ibilisi Shetani kuhakikisha kuwa anafifisha nguvu ya uimbaji ambayo ilikuwa ikikua kwa kasi sana.

Mimi na wewe tumeshuhudia migongano kati ya viongozi na Masolo(single artist) ambao waliamua kutoka katika kwaya zao na kuanza kuimba wenyewe, Baada ya kuziacha kwaya zao kauli iliyosikika ni kwamba hao ni wabinafsi huko walikokwenda wamekwenda kwa lengo la kutafuta fedha na si kumtumikia Mungu.
Mimi sina jibu la jambo hili, sijui wewe unasemaje,?
Pia katika suala hili la uimbaji wa kutumia muziki wa PlayBack tumeshuhudia ukididimiza kabisa viwango vya kwaya kubwa na kujikuta wakikosa CD ama umeme unapokatika inakuwa shida kweli kweli.
Zipo baadhi ya kwaya zimeshtuka katika jambo hili na kuanza kujishughulisha na uimbaji wa Live hata kama wakialikwa kwenye ukumbi mkubwa wa namna gani miongoni mwa kwaya hizo hapa Dar ni pamoja na Efatha, Hekima, AIC Chang'ombe na kwaya zingine.

Wengi wanasema hii ni njama ya ibilisi ya kufifisha uimbaji kwa kuwa anajua kuwa Mungu anakaa mahali pa sifa, wewe unasemaje? kwa pamoja tujadili

4 comments:

Thom said...

Asante mkuu .

kwa kweli uimbaji wa kutumia CD playback sio mzuri, sabubu mwimbaji anageuka kuwa mcheza show sauti inatoka kwenye speaker na yeye kazi yake ni kuigiza sauti , hata kama atakaa kimya bado sauti itasikika.

ni kweli kwamba kuimba kwa kutumia cd kunauwa vipaji vya wanamuziki, sababu kama utaimba na cd.
wapiga vyombo hawatakuwepo
waitikiaji hawaitajiki cd inatosha
na pia unashindwa kugundua vipaji vipya vinakuwa vimemezwa na cd

tujitahidi kuimba live

Unknown said...

Ni kweli kabisa ndugu yangu, yamkini kwaya zetu zinatakiwa kubadili mtizamo na kurudi katika njia yake, siku zote shetani anapambana na kila roho njema inayotaka kujiinua kwa ajili ya bwana

Lwaga said...

Kwanza hongera kwa kuwa na blog nzuri. Hekima Kwaya mko juu. Kuhusu mada iliyopo, mimi nadhani ni mtazamo tu. Mbona mtu unaweza kusikiliza CD au kanda na ukabarikiwa tu? Sasa si bora zaidi pale unapomuona mwimbaji mwenyewe aliyeifanya hiyo kazi akionyesha live alivyoimba? Mimi nadhani hapa kuna mambo mengi ya kuangalia. Kwanza, tukubaliane kwamba ndio kwanza tunaendelea, hatujawa na uwezo wa kuwa na wapigaji wa kutosha, vyombo vya kutosha na muda wa kutosha. Wakati mwingine afadhali kutumia playback kuliko kusubiri hao wanaopiga live wakitumia dakika hata tano wakirekebisha vyombo vyao kabla ya kuimba.
Kweli live ni live na inapendeza kuongeza kwaya na waimbaji wengi wanazidi kufanya kazi za live, likini tusiwabeze au kuwakatisha tamaa waimbaji wanaotumia playback. Ni jambo la muda tu watatoka na kuweza kufanya vizuri baadaye.
Waimbaji wote mubarikiwe.

Unknown said...

ahsante lwaga, ni kweli kabisa lakini inatupasa kumwimbia Mungu kwa ukamilifu bila kulegalega, hivyo basi, uimbaji huu wa playback kwa namna moja ama nyingine unawafanya waimbaji wakawa wavuvu na kujikuta wakipotezxa vipaji vyao kila iitwapo leo

© 2013 HEKIMA KWAYA MORAVIAN-KINONDONI . All rights resevered. Designed by Templateism