Kuna wimbo mmoja umeibwa na kwaya ya Tumain Usharika wa Sent James kanisa la Anglican pale Arusha.Wimbo huu unajulikana kwa jina la majibu ya maombi yako ndugu yalipochelewa, ukajiuliza ni wapi utapatikana msaana, basi ndugu ukumbuke upigapo magoti Mungu baba husikia ombi lako si bure, ombi lako limeandikwa katika kitabu hakika litajibiwa kwani baba mwaminifu, zungumza naye mkumbushe na mweleze kwa siri hata katikati ya watu yeye bwana husikia.
Maneno haya hakika ni faraja kubwa sana kwa sisi tulio wa kristo ambao lengo letu ni kuiona paradiso ya milele, yawezekana umekata tamaa baada ya kutumia muda mwingi kumuomba Mungu bila kupata majibu, leo Mungu anasema ombi lako lipo zungumza naye hata kwa siri yeye husikia, embu chukua hatua, yawezekana umeomba sana lakini yamkini bado hujachukua hatua ya kutekeleza maombi uliyoomba, embu chukua hatua nawe utaona matunda yake, elewa kuwa imani bila matendo imekufa
No comments:
Post a Comment