AD (728x90)

Monday, June 6, 2011

Furaha ya Mungu ikikaa nasi tutakombolewa

Mchungaji wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Kinondoni Mr Kabuka amewataka waumini wa kanisa hilo na wakristo kwa ujumla kumtumikia Mungu kwa uaminifu ikiwa ni pamoja na kuwa na furaha wakati wote kwani hiyo ndiyo ishara ya kuujenga mwili wa kristo.


Akizungumza katika ibada ya tamasha la kuchangia ununuzi wa vyombo vya Muziki, Mchungaji Kabuka alisema kuwa changamoto iliyopo kwa kanisa hivi sasa ni waumini kuishi maisha ya utakatifu yenye kulinda maadili ya kikristo siku zote.

"Maneno ya Mungu yanasema furaha ya bwana, iko ndani yetu, lakini wengi wetu tunaikosa furaha hiyo ya bwana wetu Yesu Kristo kwa kuwa tumeendelea kuyachuchumilia mambo yanayoonekana kuliko kumtafuta Mungu kwa ukaribu" alisema Kabuka.

akizungumza kuhusu vyombo vya Muziki Mchungaji huyo alisema kuwa siku zote muziki ni sehemu ya ibada, kwani hata neno la Mungu linanena waziwazi kuwa tukifika mbinguni tutamsifu mungu kwa zumari lenmye nyuzi nyingi.

Hivyo aliwataka waumini wa kanisa hilo kuelewa kuwa wanapomtolea Mungu kwa ajili ya kazi yake hawafanyi bure bali wanaujenga mwili wake, hivyo baraka zitaambatana nao wale waaminio.

Alisema kuna kila sababu kwa waumini kuishi maisha ya utakatifu siku zote, ingawa mwovu ibili ambaye ni mshtaki wetu siku zote amekuwa akitengeneza kila aina ya hila ili kuwaangusha waumini.

"Unajua upepo unapovuma umekuwa ukiwaangusha watu wengine na kujikuta wakiacha kutenda matendo yaliyo mema, ni maombi yangu kuwa muwe na amani na kupendana zaidi sana siku ya mwisho tukaonane katika paradiso ya milele"alisema Mchungaji huyo.

katika ibada hiyo Kwaya Kuu ya ushirikia huo iliongoza sifa wakifuatiwa na Hekima Kwaya, Umoja wa wakinamama, Middle kwaya pamoja na kwaya ya Havest ambayo hivi sasa inatamba na albamu yake mpya.Mungu atubamriki sisi sote.

2 comments:

Anonymous said...

Mungu awabariki sana katika huduma yenu hakika tunamuona Mungu kupitia huduma hii, endeleeni hivyo hivyo.Pia Mungu awape amani ya kweli mnapotafuta vyombo vya Muziki kumbukeni kuwa hamtoi bure bali malipo yenu yapo

Unknown said...

tunakushukuru sana ndugu yangu maoni yako kwetu sisi ni muhimu sana

© 2013 HEKIMA KWAYA MORAVIAN-KINONDONI . All rights resevered. Designed by Templateism