Baada ya kauli ya Rais Jakaya Kikwete kwamba baadhi ya viongozi wa dini wanahusika katika kufanya biashara za madawa ya kulevya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), imempa Rais masaa 48 ikimtaka awataje hadharani viongozi wa madhehebu ya dini wanaohusika na biashara hiyo
.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Makamu Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dk Valentino Mokiwa wakati jumuiya hiyo ilipokuwa ikitoa maazimio ya Mkutano wa 45 wa Halmashauri Kuu ya jumuiya hiyo iliyoketi juzi.
Askofu Mokiwa alisema kauli ya Rais Kikwete imewasikitisha kwa kuwa amewahusisha viongozi wote wa dini jambo ambalo si zuri mbele ya jamii.
" NI vema kama Rais akataja majina ya viongozi wanaohusika na na biashara hii ndani ya saa 48, akishindwa itakuwa ni aibu zaidi kwake na serikali," alisema Mokiwa.Alisema
Na kuongeza kuwa wanategemea Rais Kikwete atafanya hivyo na kinyume chake atakuwa hajawatendea haki wananchi.
Akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga, juzi kwenye ibada maalumu ya kupewa daraja la Uaskofu na kusimikwa Mhashamu Askofu John Ndimbo wa jimbo hilo, Rais Kikwete aliwaonya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini akiwataka kuacha tabia ya kushiriki biashara ya kuuza dawa za kulevya, badala yake washirikiane na viongozi wa serikali katika kudhibiti biashara hiyo haramu.
Alisema kuwa baadhi ya viongozi hao wa dini wamekuwa wakishiriki kufanya biashara ya dawa za kulevya kwa kuwafanyia mipango vijana kuwatafutia hati za kusafiria kwenda nchi za nje kwa ajili hiyo.
“Inasikitisha sana na kutisha. Biashara hii haramu sasa inawavutia hata watumishi wa Mungu, taifa letu litaharibika tusipokuwa makini katika hili, baadhi yenu tumewakamata,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment