Shusho amefanikiwa kujijengea sifa kwa mashabiki wa nyimbo za Injili ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kutokana na nyimbo zake kubeba ujumbe mzito kwa jamii, lakini ukiwa katika msingi wa neno la Mungu ambalo analiamini.Umahiri wake katika kuimba nyimbo za Injili umemuwezesha Shusho kutambulika vyema na kujinyakulia Tuzo mbalimbali ikiwemo Tuzo aliyopata wiki chache zilizopita huko Nairobi, Kenya.
Shusho alikuwa kati ya wasanii wa Tanzania waliopata Tuzo za Muziki za Afrika Mashariki na Kati (EMAS) zilizofanyika Agosti 20, mwaka huu na kushirikisha wasanii mbalimbali wa kutoka nchi nane za Afrika Mashariki na Kati.
Shusho hakika watu wanapokutizama wanamuona Mungu wetu aliye hai.Blog hii ya injili inakutakia mafanikio mema zaidi sana usimwache Yesu aende zake siku zote mtumikie Mungu wako kwa furaha nawe utakula mema ya nchi.Barikiwa
No comments:
Post a Comment