Na Peter Edson
Mchungaji mwanafunzi wa Chuo cha Thiologia cha ST Max kilichopo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam, Bi Monica Stephen Jaha, amewataka wazazi na walezi wa vijana kuwapa watoto wao elimu kwa lengo la kuliandaa kanisa lijalo ambalo kwa sasa linakabiliwa na changamoto nyingi za kiuchumi.
Pia ametoa wito kwa Vijana kuishi maisha ya utakatifu ikiwa ni pamoja na kuwatiii wazazi na walezi wao kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanatimiza wajibu wao kibiblia kwani maandiko yanasema weshimu baba yako na mama yako ili sikuzako za kuishi zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na bwana Mungu wako.
Bi Jaha alisema Kanisa la leo linatakiwa kuweka kipao mbele katika kuhakikisha kuwa inawapa elimu watoto na vijana watakaokuwa ni viongozi wa kanisa baadaye, kwani vijana wakipata elimu wataondokana na hali ngumu ya kiuchumi zaidi sana wataishi kwa amani na utulivu.
"Wazizi wangu elimu ni chanzo cha maarifa, tusipowapa watoto wetu elimu tunalibomoa kabisa kanisa la kesho, matamanio ya vijana wengi ni kuhakikisha kuwa wanakaa ndani ya kanisa wakiwa na uchumi mzuri" alisema
Alisema neno la Mungu linaeleza waziwazi kuwa Mwanangu mshike sana elimu asiende zake, hivyo kanisa linatakiwa kutambua kuwa lina wajibu katika kuchunguza na kuangalia elimu za vijana wao ili kuwakomboa na kuwasogeza karibu na uchumi.
"Vijana hawa wakijikwamua kiuchumi, kanisa litapata sadaka na malimbuko, lakini wasipokuwa na uchumi mzuri kanisa litaendelea kusuasua, inatupasa kujitoa katika jambo hili haijalishi huyu ni mtoto wako ama yule ni nani" alisema
Aidha alitoa wito kwa vijana kuishi maisha ya utakatifu yatakayompendeza Mungu na wanadamu pia, alisema vijana na waimbaji ni kama wahubiri hvyo wanatakiwa kujipanga sawasawa.
"Ninyi ni barua hivyo ni vema barua zenu zikasomeka sawasawa na jinsi mlivyo, zaidi sana yachuchumilieni yaliyombinguni ili mpate kuukulia wokovu na hatimaye kazi yenu ikaonekane mbinguni.
katika hatua nyingine vijana walisoma Risala yao kwa mgeni rasmi Dada Ester Kapalala iliyokuwa imesheheni katika kila idara zote, ambapo hoja kubwa ya vijana ilikuwa ni kuimarisha uchumi ndani ya idara kwa lengo la kutekeleza kazi za kanisa.
Naye Dada Kapalala aliwaeleza vijana kuwa wanapaswa kuishi maisha ya utakatifu na kwa wale ambao wanajijua kuwa wanatoka nje ya maadili ya kanisa wanapaswa kutengeneza ili kanisa liendelee kuheshimika na kuonekana kuwa ni kimbilio la wanyonge.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
3 comments:
mungu akubariki sana dada kweli umenena wazi kuwa pasipo uchumi imara na endelevu kwa vijana tutabaki kuwa tegemezi, amani kwako
ndiyo huyu dada mungu anamtumia tuzidi kumuombea aendelee mbele ni hazina katika kanisa
ahsante thom barikiwa sana, usisite kutushauri, barikiwa
Post a Comment