AD (728x90)

Monday, September 12, 2011

Ajali ya meli Zanzibar itukumbushe kuwa sisi ni wapitaji katika Dunia hii

Wasamaria wema wakifanya jitihada za kuokoa miili ya wahanga wa ajali ya meli ya MV Spice Islanders
Ni kweli kabisa kwamba Maandiko yanatueleza namana ya kumshukuru Mwenyezi Mungu katika kila jambo, lakini tunakila sababu ya kuwakumbuka ndugu zetu waliotutangulia,nimipango yake Mungu wetu kwani alitoa na tena ametwaa, lakini kibinadamu ni majonzi sana lakini kiroho ni faraja maana tunajua kuwa tutawakutakatika makao yetu ya milele.

Hekika kwaya kwa pamoja tunatoa pole wa wafiwa wote, hakuna mtu anayeweza kuwapa faraja ya kweli, lakini Mungu pekee ndiye mfariji wa maisha yetu, kwani hata Serikali ikifanya jitihada zote za kuhakikisha kuwa inatoa michango na kusaidia shughuli za mazishi bado uchungu upo.Mungu pekee ndiye mtetezi wa mambo yetu yote na faraja ya kweli katika maisha yet.Amani yake iwe nanyi katika kipindi hiki kigumu.

Amen

No comments:

© 2013 HEKIMA KWAYA MORAVIAN-KINONDONI . All rights resevered. Designed by Templateism